Karibu kwenye familia ya ushindi – The Game Changers.

Mimi ni Harry Mwijage, Chief Visionary Officer (C.V.O) wa timu hii ya kipekee.
Nimejitoa kwa moyo wote kuongoza harakati hii ya kuandika historia mpya kwenye biashara ya mtandao hapa Tanzania na hata nje ya mipaka yetu.

Dira yetu ni moja – Kujenga Viongozi Imara na Mamilionea wa Baadaye!
Tunaamini kuwa mafanikio si bahati; mafanikio ni mchakato wa kujifunza, kuongoza, na kuchukua hatua sahihi kila siku.

Katika The Game Changers, hatujengi timu ya wauzaji tu – tunajenga viongozi wa biashara, wahamasishaji wa jamii, na viongozi wa kifedha watakaobadilisha maisha yao na ya wengine.

Tunachojenga ni tofauti:

  • Uongozi wa kweli: Tunakuza watu kuwa viongozi wanaoweza kufundisha, kuongoza, na kujenga vizazi vya washindi.

  • Mafunzo endelevu: Kupitia Sales Coaching, Product Knowledge, na Leadership Development, kila mshiriki wetu anakua kitaaluma na kibinafsi.

  • Utamaduni wa Ushindi: Tunaamini kuwa kila mtu ndani ya timu ana nafasi ya kung’aa, na hakuna mafanikio ya mtu mmoja – mafanikio yetu ni ya pamoja.

  • Kuunda Mamilionea: Tunafundisha na kuweka misingi sahihi ya ukuaji wa kifedha, kuwezesha watu wetu kuijenga ndoto yao ya kifedha bila mipaka.

Kwa Nini Kuwa Sehemu ya The Game Changers?

Katika dunia ya leo inayobadilika kwa kasi, biashara ya mtandao ni fursa isiyo na ukomo. The Game Changers inakupa mazingira ya ukuaji, uungwaji mkono wa kitaalamu, na jukwaa la kujijenga kutoka ndoto hadi uhalisia.

Hapa, kila mwanachama anathaminiwa, anapewa mafunzo bora, na anaandaliwa kuwa mchezaji wa kimataifa kwenye ulingo wa biashara na maisha.


Upo Tayari Kupindua Meza?
Badilisha maisha yako.
Badilisha maisha ya wengine.
WE ARE THE GAME CHANGERS!
SISI NI WASHINDI – KUSHINDA NI JADI YETU!