Safari ya Zachary: Kutoka Kwa Mateso ya Ajira Hadi Kwenye Maisha ya Ndoto Kupitia BF SUMA

Naitwa Zachary J. Kulaya. Kabla ya kufika nilipo sasa, maisha yangu yalikuwa ya mateso, hofu, na sintofahamu. Nilikuwa muajiriwa kwenye kampuni ya kubeti ya Meridian. Nilifanya kazi kwa muda mrefu, bila mapumziko, bila sikukuu wala likizo. Maisha yalikuwa ya taabu — mshahara mdogo, hofu ya kufukuzwa kazi kila wakati, na madeni kila duka nililopita kutokana na mahitaji ya familia ambayo yalizidi uwezo wangu wa kipato.

Nilipoamua kuacha kazi, niliingia kwenye dunia ya ujasiriamali. Nilijaribu kuuza vinyago, lakini janga la corona lilikuja na biashara ikafa. Sikukata tamaa — nikaamua kuuza viatu. Lakini hata hiyo biashara haikudumu. Mahitaji yalizidi mtaji, nikaishiwa tena.

Ndipo nilipokutana na mkombozi wa maisha yangu, kupitia kiongozi wangu mpendwa Harry Mwijage. Mwaka 2019 kupitia ujumbe wa Facebook, alinijulisha kuhusu BF SUMA. Sikuchukua hatua haraka, jambo ambalo najutia hadi leo. Lakini tarehe 15/10/2021, niliamua kujiunga rasmi na BF SUMA — na huo ukawa mwanzo wa maisha mapya.

Kupitia BF SUMA:

  • Nimepata tumaini jipya la maisha bora. Familia niliyoipoteza kwa sababu ya ukosefu wa fedha, sasa imeanza kujengwa upya.
  • Nimeondokana na madeni yote. Leo hii, sina deni hata moja dukani.
  • Nimeweza kusafiri kimataifa:
    • 2023 nilisafiri kwenda South Africa
    • 2024 nikapata nafasi ya kwenda Dubai
    • 2025 ninajiandaa safari ya tatu kurudi South Africa, huku nikijiandaa kushinda gari kupitia mfumo huu wa biashara.
  • Namiliki duka la simu, jambo ambalo sikuweza hata kulifikiria zamani.
  • Nimejenga nyumba ya kuishi mimi na watoto wangu.
  • Namiliki heka moja ya kiwanja huko Kisarawe.
  • Na kwa sasa, kupitia mfumo wa BF SUMA, natarajia kuingiza zaidi ya Dola 15,000 kila mwezi — jambo ambalo halikuwezekana hata kwenye biashara zangu zote za nyuma.

Leo hii, najivunia kusema kwamba BF SUMA ni kubwa kuliko biashara zote nilizowahi kufanya. Imekuwa daraja la kutoka kwenye maumivu ya ajira hadi kwenye mafanikio ya kweli. Kwa yeyote anayesoma hadithi yangu — usiache kuchukua hatua. Maamuzi yako leo yanaweza kubadilisha maisha yako milele.