Kwa majina naitwa Madina Yassin Foka. Kabla ya kujiunga na BF SUMA, nilikuwa nafanya kazi katika kampuni ya CELLO kama kiongozi. Kazi yangu kubwa ilikuwa kuwaelekeza wafanyakazi wapya jinsi ya kuuza na kupromoti bidhaa za kampuni hiyo. Ingawa nilikuwa na nafasi nzuri ya uongozi, changamoto zilikuwa nyingi.
Moja ya changamoto kubwa ilikuwa kutembea umbali mrefu kwa masaa zaidi ya nane nikibeba bidhaa, na mwishowe kurudi nazo ofisini bila kuuza hata moja. Hiyo ilimaanisha kurudi nyumbani bila mshahara, bali nauli tu. Kama msichana niliyekuwa najitegemea, hali hii ilionekana kama mateso makubwa sana kwangu. Ukosefu wa malipo ya uhakika ulifanya maisha kuwa magumu sana.
Mwaka 2021 mwezi wa pili, maisha yangu yalianza kubadilika. Nilikutana na BF SUMA kupitia kiongozi wangu wa zamani aitwaye Braison. Tulikutana naye kule CELLO, ambapo nilikuwa mwalimu wake wa biashara. Baada ya yeye kushindwa kuendelea na CELLO, alijiunga na BF SUMA na alipoona mafanikio yake ya haraka, alinipigia simu na kunishirikisha fursa hiyo. Niliamua kumuamini, nikiwa nimechoka na maisha ya mateso. Nilipoelewa faida za BF SUMA, sikusita – nilijua hii ni nafasi sahihi kwangu.
Kujiunga na BF SUMA kulibadilisha maisha yangu kwa asilimia 100. Kwa mara ya kwanza, niliona uhuru wa kifedha na kiafya. Kupitia bidhaa za BF SUMA, nilimsaidia mama yangu aliyekuwa anasumbuliwa na goita – sasa ni mzima kabisa. Leo hii, kipato changu hakishuki chini ya milioni 1.5 kwa mwezi.
Sio hivyo tu – nilijiwekea malengo ya mwaka mmoja kuanzia 1/1/2023 hadi 1/1/2024 ya kumjengea mama yangu nyumba. Kupitia mauzo ya rejareja na bonasi nilizopata BF SUMA, niliweza kutimiza lengo hilo mwezi wa pili mwaka 2024. Nyumba hiyo imenigharimu milioni 25, lakini furaha ya kumuwekea mama wangu makazi bora haiwezi kupimwa kwa pesa.
Zaidi ya hayo, niliambiwa kuhusu tuzo ya kusafiri nje ya nchi kwa wale wanaofanya vizuri. Sikuwahi kusafiri nje ya Tanzania, hivyo nikajiwekea lengo la kushinda tuzo hiyo. Kwa juhudi na bidii, nilitangazwa kuwa mshindi mwaka 2024 mwezi wa 11 – ndoto yangu ya kusafiri nje ya nchi ikatimia!
Na bado sijaishia hapo. Ndani ya miaka mitano ijayo, nina malengo makubwa kupitia BF SUMA:
- Kwanza, kushinda gari lenye thamani ya milioni 30.
- Pili, kuwa na ofisi kubwa mimi pamoja na timu yangu ya mafanikio.
- Na tatu, kuhakikisha kipato changu hakishuki chini ya milioni 10 kwa mwezi.
Ninayo imani kuwa, kwa bidii, uaminifu, na kujitoa, BF SUMA siyo tu biashara, ni daraja la ndoto kutimia. Mimi ni ushuhuda hai wa mafanikio hayo!