Anasimulia:
Naitwa Getrude George Malanga. Kwa moyo wa shukrani na furaha isiyo na kifani, namshukuru Mungu kwa kunitambulisha na kuniongoza kwenye maisha ya mafanikio kupitia BF SUMA. Kwangu, BF SUMA siyo tu kampuni—ni mkombozi, daraja lililoniwezesha kuvuka kutoka kwenye ndoto hadi kwenye uhalisia wa maisha yaliyojaa heshima, fursa, na mafanikio.
Siku ya kwanza niliposikia kuhusu BF SUMA, sikujua kama ilikuwa ndio mwanzo wa mabadiliko ya maisha yangu. Nilielezwa kuhusu mfumo wake, jinsi unavyogusa maisha ya watu, na fursa kubwa zinazopatikana ndani yake. Niliposikia hayo, moyo wangu ulijawa na matumaini mapya. Nilijua huu ulikuwa mwanzo wa safari mpya.
Kupitia BF SUMA, maisha yangu yalibadilika hatua kwa hatua. Leo hii, ninaheshimiwa, siyo tu katika familia yangu, bali pia na jamii inayonizunguka. Nimepata tuzo mbalimbali za kutambua juhudi na mafanikio yangu, jambo ambalo lilikuwa kama ndoto hapo zamani.
Safari yangu kupitia BF SUMA imenifikisha mbali zaidi ya mipaka ya Afrika. Nimevuka mabara—nimeitembelea Dubai, Hongkong, Thailand—mahali ambapo zamani nilikuwa naangalia tu kwenye luninga. Kwa sasa, kusafiri kimataifa ni sehemu ya maisha yangu ya kila mwaka, na yote haya ni kwa neema ya BF SUMA.
Nakumbuka maisha yangu kabla ya BF SUMA—nilikuwa napanda daladala, nikihangaika kama watu wengine wengi. Leo hii, ninamiliki gari langu lenye thamani ya zaidi ya milioni thelathini. Ni tuzo halisi ya juhudi zangu kupitia mfumo wa BF SUMA. Hili ni jambo ambalo linanifanya nitabasamu kila ninapoangalia nyuma nilikotoka.
Kutoka kwenye kutegemea nguvu zangu peke yangu na kuishi maisha yasiyo na uhakika, sasa naishi maisha yenye dira, uthabiti na matumaini. Nimekuwa daraja la mafanikio kwa wengine pia. Nimewasaidia watu wengi kufikia kipato cha laki tano hadi milioni moja kwa mwezi. Mpaka sasa, nimefanikiwa kuandaa washindi watatu wa safari za kimataifa, nao pia wameweza kufika Dubai kupitia timu yangu.
Nikiangalia mbele, miaka mitano ijayo naona picha ya Getrude Malanga kama kiongozi mkubwa barani Afrika. Jina langu litatajwa miongoni mwa wanawake wanaofanya mambo makubwa, na halitakosekana kwenye orodha ya waliobadilisha maisha ya maelfu. Natarajia kuona washindi wasiopungua kumi wa safari za kimataifa kutoka katika miguu tofauti ya timu yangu, pamoja na magari matatu mapya kwa mwaka ujao.
Nina ndoto kubwa zaidi: kila mwaka kuona watu zaidi kutoka timu yangu wakishinda magari na safari, kutengeneza viongozi wa SDL na SCL, na mimi mwenyewe kuwa SCL ndani ya miaka miwili ijayo—nikivuka zaidi ya milioni 60 kwa mwezi.
Ninaposema “I LOVE BF SUMA”, si maneno tu—ni sauti ya moyo wangu wa shukrani kwa mabadiliko ya kweli yaliyoleta maana katika maisha yangu.