Naitwa Fadhili Mbogo. Kama kijana yeyote mwenye ndoto kubwa na tamaa ya mafanikio, nilianza safari yangu ya kutafuta mafanikio nikiwa bado shuleni. Mwaka 2010, nikiwa kidato cha tano, nilijiunga kwa mara ya kwanza na kampuni ya biashara ya mtandao. Ingawa nilikuwa na ari, sikufanikiwa kwa sababu ya kukosa ujuzi wa kutosha.

Mwaka uliofuata, 2011, nikiwa mwanafunzi wa Chuo cha IFM, nilijitahidi kuanzisha biashara kadhaa, lakini bado sikufanikiwa—safari hii sababu ilikuwa ni ukosefu wa muda wa kusimamia biashara hizo ipasavyo kutokana na majukumu ya chuo. Nilipohitimu na kupata shahada yangu ya kwanza katika Teknolojia ya Habari (BSc IT), nilipata ajira kwa haraka katika moja ya kampuni kubwa ya simu nchini.

Kupitia mshahara wangu, nilianzisha biashara mbalimbali: chakula, ufugaji, kilimo, na store ya mazao—ambazo kwa pamoja ziligharimu zaidi ya milioni 150 za Kitanzania. Kwa bahati mbaya, zote zilifeli. Sababu kuu? Ukosefu wa usimamizi wa karibu na muda wa kuzisimamia.

Kwa upande mwingine, ajira haikuniridhisha.

  1. Nilihisi ninatumia muda mwingi kuinufaisha kampuni ya watu wengine.
  2. Malipo hayakuendana na juhudi na muda niliokuwa naweka.
  3. Hakukuwa na uhakika wa kuongeza kipato hata kama ningefanya kazi kwa bidii—mambo yalifuata utaratibu mgumu na wa polepole.

Nilianza kuamini kwamba ajira haina uwezo wa kutimiza ndoto zangu. Ndipo mwaka 2018, marafiki zangu wawili, Mwijage na Jose, walinieleza kuhusu fursa ndani ya kampuni ya BF SUMA. Ingawa sikuona matokeo ya haraka, nilivutiwa na namna bidhaa zao zilivyokuwa zinaleta matokeo kwa watumiaji, huku mimi nikipata faida kutokana na mauzo.

Kupitia mfumo wa malipo wa BF SUMA, mwaka 2022 nilishinda gari jipya aina ya Subaru XT lenye thamani ya milioni 42 – kitu ambacho singeweza kukipata kwa kutegemea mshahara wa ajira. Mwaka uliofuata, 2023, nilitimiza ndoto ya kusafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza, safari iliyogharamiwa kikamilifu na kampuni kwenda Afrika Kusini.

Leo hii, kupitia bonus ya kampuni, naweza kufanya shughuli zangu nyingine bila kuvuruga kazi yangu ya BF SUMA. Naamini kabisa kwamba kupitia fursa hii, ndoto zangu zote ambazo nilikuwa naziota tangu ujana zitafikia kutimia.

Katika miaka mitano ijayo, nimejiwekea malengo makubwa ambayo naamini nitayafikia:

  1. Kumaliza mfumo wa malipo na kuwa SCL (Senior Center Leader) huku nikipokea bonus ya zaidi ya milioni 70.
  2. Kutengeneza SCL wapya watano.
  3. Kusaidia watu 20 kushinda magari.
  4. Kuwezesha safari 100 za nje ya nchi kwa washiriki wenzangu.
  5. Kumiliki nyumba ya kisasa Masaki.
  6. Kumiliki Land Cruiser LC 300.
  7. Kumiliki mashamba hekari 100,000.
  8. Kumiliki helikopta binafsi.
  9. Kujenga kiwanda cha kuzalisha unga.
  10. Kujenga kituo cha kulea watoto yatima—ambapo nitakuwa baba yao mwenyewe.
  11. Kujenga msikiti mmoja kila mwaka kama sadaka ya kudumu.

Fadhili Mbogo si jina tu, ni ushuhuda wa kwamba kijana mwenye ndoto, nia na bidii anaweza kuvuka vizingiti vyote na kufanikisha maisha ya thamani na athari chanya kwa jamii.