Hadithi ya Mafanikio ya Bariki Nikanoli Masatu: Kutoka Sokoni hadi Jukwaa la Mafanikio

Naitwa Bariki Nikanoli Masatu. Mimi ni mshauri wa biashara (Business Coach) na mhitimu wa elimu ya juu kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Lakini safari yangu haikuwa laini, bali imejaa milima na mabonde yaliyoniandaa kuwa mtu niliye leo.

Wakati nikiwa chuoni, sikuishia kusoma tu – nilianza ujasiriamali kwa kuuza matunda, viatu, mitumba ya nguo, hadi kufungua mgahawa mdogo. Nilijifunza mapema kuwa mafanikio hayaji kwa kusubiri bali kwa kuchukua hatua.

Baada ya kuhitimu, ajira haikupatikana mara moja. Hapo ndipo nilianza biashara ya kununua mazao kama mchele na viazi kutoka Mbeya na kuyasafirisha hadi Dar es Salaam. Biashara hii ilijaa furaha na changamoto kwa pamoja. Kuna nyakati nilipata faida, lakini pia nilipoteza – bidhaa kuharibika, kutapeliwa na madalali, na wakati mwingine kuibiwa. Ilikuwa ni shule ya maisha.

Muda ulivyozidi kusonga, nilipata ajira kwenye kampuni ya Shipping na Clearing & Forwarding. Lakini mshahara ulikuwa mdogo – shilingi 600,000 tu kwa mwezi – huku nikikosa muda wa kusimamia biashara zangu. Baada ya kutafakari kwa kina, niliamua kuachana na ajira hiyo.

Lakini mapenzi yangu kwa biashara hayakufa. Nikakumbuka kuhusu BF SUMA – kampuni ya kimataifa ya bidhaa za afya. Mama yangu mkubwa Belnais na kaka yangu Joseph waliwahi kuniingiza kwenye semina kuhusu biashara hii nikiwa chuoni. Mwaka 2020, niliamua kuanza kufanya biashara ya Bfsuma kwa muda wa ziada.

Miezi mitano baadaye, nikafanya uamuzi wa maisha – kuacha kazi rasmi na kujiunga full time na Bfsuma. Niliona kipato chake kilikuwa kikubwa kuliko ajira, na zaidi ya fedha, niliona fursa ya kusaidia wengine.

Leo, ninaweza kusema kwa fahari kwamba Bfsuma imenibadilishia maisha. Naweza kuhimili mahitaji ya familia yangu, kuwasomesha wadogo zangu, na nimemjengea mama yangu nyumba. Nimesafiri nje ya nchi – mara mbili Dubai na Abu Dhabi, pia South Africa. Mwaka 2023, nilishinda gari aina ya Harrier nyeupe yenye thamani ya shilingi milioni 35 (TZ495 EDZ).

Lakini haya yote ni mwanzo tu.

Dira Yangu ya 2025 – 2030:

  • Kuwa SCL mwenye GPV 300,000+ na kipato cha milioni 60+ kila mwezi
  • Kuingia kwenye Top 4 earners wa Bfsuma
  • Kununua Ford Ranger ya shilingi milioni 200
  • Kushinda nyumba ya Bfsuma ya thamani ya milioni 560
  • Kuwezesha SDL 10 ndani ya timu yangu
  • Kusaidia watu wengi kushinda magari na safari za kimataifa kila mwaka
  • Kujenga apartments za thamani ya bilioni 1
  • Kuanzisha ofisi kuu ya “The Lions Team Headquarters”

Ee Mwenyezi Mungu, nipe neema, hekima na uvumilivu kuifikia ndoto hii. Najua kwa juhudi na maombi, kila kitu kinawezekana.