MATATIZO YA MIFUMO YA MWILI TUTAYOJINFUNZA NA BIDHAA ZAKE
- Mfumo wa damu
- Mfumo wa viungo na mifupa
- Mfumo wa wanaume
- Mfumo wa wanawake
- Mfumo wa Mmeng’enyo wa chakula
- Jinsi ya kupunguza Uzito, Nyama Uzembe na Mafuta mwilini
- Magonjwa mbalimbali na mchanganyiko wa bidhaa (tibalishe) zake mbadala
Mpaka sasa BF SUMA ni kampuni ya kiafya inayoongoza katika utengenezaji, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa bora za kiafya, Duniani.
Kampuni imejikita katika kutengeneza bidhaa za kiafya za asilia/mitishamba zenye ubora wa hali ya juu kwa kutumia Teknolojia zilizoendelea na pia kutoa huduma nzuri.
Hiki kitabu hakijakusudiwa kuwa mbadala wa dawa au ushauri wa Madaktari.
Imekusudiwa kumsaidia msomaji aweze kupata taarifa za ziada zitakazomsaidia kuishi maisha ya kiafya na kufanya mabadiliko inapobidi.
Msomaji anatakiwa kumshirikisha daktari wake,kila mara kuhusu afya yake na haswa kwa hali/dalili zinazoweza kujitokeza zinazohitaji uchunguzi na matibabu ya kidaktari.
Kitabu hiki kimetengenezwa mahususi kwa ajili ya kumwezesha mtu wa kawaida kabisa kujua umuhimu juu ya Afya yake. Namna ambavyo mifumo mbalimbali ya mwili hufanya kazi na namna ambavyo anaweza kuathiriwa na mtindo wa maisha.
Ifahamike kwamba mlipuko au kujitokeza kwa magonjwa mengi kumesababishwa na mtindo wa maisha ambao umechangiwa na mabadiliko ya Teknolojia ambayo yamepelekea hata umri wa kuishi kuwa mfupi (life expectance) ambapo imesababishwa na madhara yanayotokana na Teknolojia kama vile mbolea za kukuzia vyakula, mifugo pamoja na mionzi ya mawasiliano nk.