Katika hatua kubwa ya kuimarisha huduma na kuleta bidhaa karibu zaidi na wajasiriamali na wateja, Game Changers imezindua rasmi subshops katika mikoa mitano mikubwa nchini Tanzania – Dodoma, Arusha, Zanzibar, na Njombe, chini ya duka la Dar es Salaam,.
Subshops hizi ni sehemu ya mpango maalum wa kuongeza upatikanaji wa bidhaa bora za afya na lishe, na kutoa msaada wa karibu zaidi kwa distributors wanaokuza biashara zao kupitia mfumo wa masoko wa BF Suma.
📍 Dodoma – Kisasa:
Moyo wa siasa na maendeleo sasa unapata kituo cha nguvu cha Game Changers. Distributors wa BF Suma wanaweza sasa kupata bidhaa kwa urahisi zaidi, kuhudhuria mafunzo, na kujenga timu zao kwa kasi katika mji huu unaokua kwa haraka.
📍 Arusha – Mega Complex:
Katika jiji la kitalii, subshop ya Arusha inaleta hamasa mpya kwa wajasiriamali na vijana wanaotafuta fursa za kifedha. Mafunzo ya uongozi na maonyesho ya bidhaa yatafanyika mara kwa mara kusaidia ukuaji wa biashara.
📍 Dar es Salaam – Ilala:
Dar es Salaam – kitovu cha biashara Afrika Mashariki – Kina Duka la kisasa na kuu kwa mengine linalowahudumia distributors. Hapa, wanachama wanapata bidhaa kwa haraka, huduma za usaidizi wa biashara, na fursa ya kushiriki katika warsha na semina za kipekee.
📍 Zanzibar – Kwa Mchina Mwanzo:
Fursa mpya zimefika visiwani! Zanzibar sasa ina subshop inayowezesha upatikanaji wa bidhaa na elimu ya biashara ya mtandao, ikihamasisha ukuaji wa haraka wa timu za Game Changers ndani ya ukanda wa visiwa.
📍 Njombe – Chaugingi:
Katika nyanda za juu kusini, Game Changers wameweka alama yao Njombe. Wajasiriamali wa eneo hili sasa wanapata msaada wa karibu zaidi kwa kukuza biashara zao na kujifunza mbinu bora za mauzo na uongozi.
Subshops Hizi Zitatoa Huduma zifuatazo:
-
Upatikanaji wa bidhaa za BF Suma kwa urahisi zaidi.
-
Usajili wa wanachama wapya.
-
Mafunzo ya mara kwa mara kuhusu bidhaa na biashara.
-
Ushauri wa maendeleo ya timu na mikakati ya kuuza.
Kwa subshops hizi, BF Suma Game Changers inaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya biashara ya mtandao nchini Tanzania, ikiwapa washiriki wake msaada wa karibu zaidi, fursa nyingi zaidi, na njia za haraka kufikia mafanikio.
Kwa BF Suma Game Changers, Hii Ni Zaidi Ya Biashara – Ni Harakati Ya Kuinua Viongozi Wa Kesho!