Hadithi ya Mafanikio ya Hamisa Mbogo: Kutoka Kutembea kwa Miguu Hadi Kuendesha Gari la Ndoto

Naitwa Hamisa Mbogo, ni mama wa watoto watatu na pia ni mke wa mtu. Safari yangu ya maisha haikuwa rahisi, lakini kwa neema ya Mungu na maamuzi sahihi, leo nina sababu ya kutabasamu.

Miaka kadhaa nyuma, nilipata ajira kupitia rafiki yangu Phina kwenye kampuni moja (tuitaje Kampuni X) kama afisa mauzo na masoko. Lakini kazi hiyo ilikuwa na changamoto nyingi sana – tulilipwa tu pale tu tulipofanikiwa kuuza. Hakukuwa na mshahara wa uhakika, na hiyo ilinipa wakati mgumu sana kama mama na mke mwenye majukumu.

Siku nyingine, tulikuwa tunafanya kazi kwa miguu, tukitembea mitaani na kufanya promotion kwenye magari, mikoani na hata kwenye maeneo yenye watu wengi – lakini bado malipo yalitegemea uuzaji tu. Kila siku ilikuwa ni vita ya kuhakikisha napata hata mia ya kula.

Mwaka 2019, maisha yangu yalipata mwanga. Ndugu yangu Fadhili Mbogo alinishirikisha kuhusu fursa ya biashara ya BF Suma. Nilikataa mara ya kwanza, ya pili na hata ya tatu, lakini alivyoendelea kuniambia kwa upendo na kunieleza mafanikio yake, hatimaye nilikubali kuisikiliza.

Moja ya ndoto niliyoibeba kwa muda mrefu ilikuwa ni kumiliki pesa ya kutosha kwenye wallet yangu, kuwa na uhuru wa kifedha, na kupata usafiri wangu binafsi. Ndoto hizi zote nilikuwa nimezipiga kambi kwenye moyo wangu. Na sasa naweza kusema – NAMSHUKURU MUNGU.

Kupitia BF Suma, mwaka 2021, nilipata nafasi ya kwenda kwenye safari yangu ya kwanza nje ya nchi – Dubai. Niliona dunia kwa jicho jipya, nikakutana na watu kutoka mataifa mbalimbali, na nikajifunza mengi kuhusu maisha na biashara.

Mwaka 2022, ndoto yangu nyingine ilitimia – nilimiliki gari langu la kwanza, aina ya Nissan Murano mpya kabisa, rangi nyeusi, lenye thamani ya takriban milioni 30. Gari ambalo kila nililolitazama nilikumbuka maisha ya kutembea kwa miguu nikiwa kwenye kampuni ya zamani.

Leo hii, nina imani kuwa miaka mitano ijayo, kupitia BF Suma:

  • Nitamiliki nyumba nzuri
  • Nitasafiri nchi nyingi duniani
  • Nitamiliki apartments Dar es Salaam na Dodoma
  • Nitakuwa na biashara zangu na kipato changu kinachoingia bila wasi wasi

Mpaka sasa, BF Suma imenisaidia kupata pasipoti yangu, kusafiri nchi mbalimbali, na kujenga kipato chenye uhakika.

Sasa namiliki gari langu mwenyewe, Nissan Murano mpya kabisa kupitia jasho na maarifa ya BF Suma.

Kwa kweli, BF Suma imenipa hadhi, matumaini mapya, na uhuru wa kifedha. Kama niliweza kutoka kwenye maisha ya kutembea mtaani hadi leo kuendesha ndoto zangu – basi na wewe unaweza.

Hamisa Mbogo – Mshindi, Mthubutu, na Mshuhuda wa Mabadiliko ya Kweli.
#BFsumaSuccess #GameChanger #HadithiYaUkweli