NJIA YA KUTOKA KWA MATESO HADI UHURU WA KWELI
Jina langu ni Seif Ally, mzaliwa wa Bukoba Mjini, mkoa wa Kagera. Nilikuja Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu katika Chuo cha Biashara (CBE) nikiwa na ndoto ya kuendesha maisha bora kupitia taaluma ya Business Administration (BA). Baada ya kuhitimu, nilianza safari ya ajira – nilifanya kazi kwenye kampuni kubwa ya bima hapa Tanzania na pia kwenye kampuni ya clearing and forwarding mara mbili.
Hata hivyo, maisha ya ajira hayakunipa kile nilichokuwa natafuta. Nilikosa uhuru wa muda, niliishi kwa wasiwasi kila mara bosi alipokua ofisini, na mara nyingi nilifokewa bila sababu ya msingi. Nakumbuka kuna siku tulipingana vikali na bosi wangu kutokana na namna alivyoniamrisha kama mtoto. Ndipo nilianza kujiuliza: “Hivi maisha haya ndiyo ndoto niliyoifuata chuoni?”
Ndipo nikakutana na BF SUMA mwaka 2019 nikiwa bado kwenye ajira. Mwanzoni nilichukulia kama kazi ya kawaida tu, nikaifanya kama part-time. Lakini baada ya miezi sita tu, nikagundua kuwa BF Suma inanilipa zaidi ya kazi yangu rasmi. Hapo ndipo nilichukua uamuzi wa maisha – nikaacha ajira na kuamua kufanya BF Suma full-time.
Kupitia BF Suma:
- Nimepata dira ya maisha – najua nilikotoka na ninakokwenda.
- Nimepata mke bora – mpenzi wangu ambaye sasa ni mama wa watoto wangu nilikutana naye kupitia biashara hii.
- Nimepata uhuru wa kifedha – tofauti na zamani ambapo nilikua “choka mbaya,” sasa najimudu na najivunia maisha ninayoishi.
- Nimesafiri Dubai mwaka 2024 – safari ya kifahari niliyoipata kupitia ushindi wa mfumo wa BF Suma bila kutoa hata mia. Ilikuwa ni safari ya ndoto, ya starehe na kuthaminiwa.
Zaidi ya yote, BF Suma imenitambulisha kwa watu wenye upendo, heshima, na moyo wa kusaidiana. Tumejenga familia ya watu wanaopigania mafanikio ya kila mmoja. Kwa kweli, biashara hii imenitoa kwenye maisha magumu ya awali na kunipa fursa mpya ya kutimiza ndoto zangu.
NDOTO ZANGU MIAKA 5 IJAYO:
- Kusaidia mamia ya wanachama kupata magari na safari kubwa duniani.
- Kumiliki majumba, magari ya kifahari, hisa kwenye makampuni, na mashamba zaidi ya hekari 100.
- Kuwa na familia yenye furaha, yenye afya njema, na kipato cha kuaminika.
BF Suma sio tu biashara – ni njia ya maisha.
Ni daraja la kutoka kwenye umasikini hadi kwenye utajiri, kutoka kwenye hofu hadi kwenye uhuru, kutoka kwenye ndoto hadi kwenye uhalisia.
#HadithiYaMabadiliko
#GameChanger
#FromStrugglesToSuccess
#BFSUMAChampion