Hii ni hadithi ya Jackline George Andrea, mama wa mtoto mmoja, ambaye alipitia mabadiliko makubwa ya maisha kutoka kuwa mjaajiri hadi kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio kupitia biashara ya mtandao ya BF Suma.
Kwa mwanzo, Jackline alikuwa akiishi maisha ya kawaida akiwa mjaajiri katika kampuni fulani. Aliishi maisha ya kawaida, akiwa na malengo ya kufanya kazi kwa bidii ili aendelee na familia yake. Hata hivyo, hali hiyo ilimfanya ajikute anafanya kazi nyingi bila kuona tija kubwa.
Kama wengi, Jackline alikuwa na shaka kuhusu biashara za mtandao, hadi alipojifunza kupitia mdogo wake, Getruda Malanga. Getruda alishinda safari ya kwenda Dubai kupitia BF Suma, jambo ambalo lilimshangaza Jackline kwa kiasi kikubwa. Hapo ndipo alipojua kuwa biashara ya mtandao inawezekana na anaweza pia kufanikiwa. Alianza kwa kutumia muda wake wa ziada kufanya biashara hii bila kuathiri kazi yake ya kawaida, lakini aliweza kuona mabadiliko makubwa katika mapato yake.
Jackline alishuhudia mafanikio makubwa akiwa kwenye BF Suma. Aliingiza pesa nyingi kuliko alivyokuwa akipata kutoka kwenye ajira yake. Baada ya kuona mafanikio ya mdogo wake, Getruda, ambaye alishinda gari la thamani ya milioni 30, Jackline alijua kuwa sasa ni wakati wa kufanya maamuzi makubwa. Aliamua kuacha kazi yake ya ajira ili kujikita kikamilifu kwenye biashara ya BF Suma.
Kwa msaada wa viongozi wake, Jackline alifanikiwa kushinda safari yake ya kwanza ya kwenda Dubai, jambo ambalo hakuwahi kufikiria. Safari hii ilimfundisha mengi na kumwezesha kufungua milango ya mafanikio. Mwaka ujao, Jackline anajiandaa kwenda South Africa kwa safari yake ya pili na anaamini kuwa atachukua tuzo ya gari, kama vile alivyohahidiwa na BF Suma.
Kwa miaka mitano ijayo, Jackline anatarajia kuwa mbali na BF Suma. Anapanga kugusa maisha ya watu wengi kiuchumi na kiafya, akisaidia timu yake kuongeza mapato ya kuanzia milioni 10 kila mwezi. Anapanga kuwa na mapato ya kila mwezi yasiyopungua dola za Kimarekani 8000, kumiliki gari ya ndoto yake, Range Rover Discovery yenye thamani ya milioni 80, na pia kumiliki nyumba yenye thamani zaidi ya milioni 100.
Jackline anashukuru kwa kila hatua aliyoipitia kupitia BF Suma. Biashara hii imemuwezesha kulipa kodi ya nyumba, kumsaidia mtoto wake kupata elimu nzuri, na kusaidia familia yake kwa kukidhi mahitaji muhimu. Kwa hakika, kupitia biashara hii, maisha yake yamebadilika kabisa na anaamini kuwa anajiandaa kufika mbali zaidi.
Hadithi ya Jackline ni ushahidi wa nguvu ya kuamini katika fursa mpya na kujitolea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo makubwa.