Naitwa Margreth Deus Samburu. Mimi ni mke na mama wa watoto wawili. Zaidi ya hilo, ni muuguzi na mkunga niliyesajiliwa rasmi na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC). Nilianza kazi yangu katika maduka ya dawa na baadaye nikapata ajira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Pwani.

Licha ya taaluma yangu, maisha ya ajira hayakuwa mepesi. Nilikuwa nakosa uhuru wa muda – nilishindwa kuhudhuria misiba, vikao vya familia, hata sherehe muhimu. Kila siku nilivaa sare za kazi, mshahara niliokuwa napata haukuwa na uwiano na kazi niliyokuwa nafanya. Katika duka la dawa nilikuwa nalipwa 150,000 Tsh, tena kwa kuchelewa, na hospitalini nilikuwa napata 680,000 Tsh. Mbaya zaidi, hata ukiwa na sababu ya msingi, kama kosa litokee kwa mgonjwa, bado unakumbwa na barua na hatua kali za kinidhamu.

Maisha yakaanza kubadilika mwaka 2021, mwezi wa Aprili, nilipojiunga na kampuni ya BF Suma kupitia rafiki yangu tuliyeabudu pamoja kanisani. Hapo ndipo safari mpya ilipoanza.

Kupitia BF Suma, ndoto zangu zilianza kutimia. Leo hii, ninasafiri nje ya nchi kila mwaka – jambo ambalo nilikuwa naota tu zamani. Kipato changu ni endelevu, na kimekuwa maradufu ya kile nilichokuwa napata nikiwa mwajiriwa. Nimeweza kununua kiwanja na kujenga nyumba yangu, ambapo ujenzi umefikia asilimia 70. Aidha, nawasomesha wadogo zangu mapacha, waliopo mwaka wa pili chuoni, kwa kuwalipia ada ya Tsh 2.7 milioni kila mwaka.

Nina ndoto kubwa zaidi. Ndani ya miaka mitano ijayo, naamini kabisa kuwa kupitia BF Suma nitafanikiwa:

  • Kumiliki gari langu aina ya Range Rover nyekundu, lenye thamani ya zaidi ya milioni 70.
  • Kuongeza kipato changu hadi milioni 15 kwa mwezi.
  • Kumiliki ofisi yangu mwenyewe pamoja na timu ya wasaidizi wangu.

Hii ndiyo hadithi yangu – ya kutoka kwenye kizuizi cha ajira ya kawaida, hadi kuwa mwanamke huru, mwenye dira, ndoto na mafanikio kupitia fursa ya BF Suma.